728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, June 26, 2016

    URENO YATINGA ROBO FAINALI EURO 2016,TIMU ZAIRUDIA REKODI YA MWAKA 1980

    Lens,Ufaransa.

    URENO imekuwa timu ya tatu kufuzu Robo Fainali ya Michuano ya Euro 2016 baada ya Usiku huu Kuifunga Croatia bao 1-0 katika Mchezo Mkali uliochezwa Katika Uwanja wa Stade Bollaert-Delelis ulioko Mjini Lens,Ufaransa.

    Bao pekee la Mchezo huo uliolazimika Kuchezwa kwa dakika 120 limefungwa kichwa dakika ya 117 na Ricardo Quaresma aliyekuwa ameingia uwanjani kuchukua nafasi ya Joao Mario.

    Quaresma alifunga bao hilo baada ya kuuwahi mpira wa Cristiano Ronaldo uliookolewa na Kipa wa Croatia, Subasic na kufunga akiwa hatua chake karibu na lango.

    Aidha Mchezo huo umeweka rekodi ya kuwa mchezo wa kwanza kuchezwa dakika zote 90 bila ya timu zote kupiga shuti lililolenga lango ( shot on target) tangu mwaka 1980.

    Kwa matokeo hayo sasa Ureno itacheza na Poland Katika mchezo wa Robo Fainali utakaochezwa siku ya Alhamis huko Marseille.

    VIKOSI

    CROATIA (4-2-3-1): Subasic, Srna, Corluka (Kramaric 120), Vida, Strinic, Modric, Badelj,Brozovic, Rakitic (Pjaca 110), Perisic,Mandzukic (Kalinic 88)

    URENO (4-2-3-1): Rui Patricio, Soares,Pepe, Fonte, Guerreiro, Joao Mario (Quaresma 87), Adrien Silva (Danilo 108),Carvalho, Andre Gomes (Renato Sanches 50),Nani, Ronaldo

     

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: URENO YATINGA ROBO FAINALI EURO 2016,TIMU ZAIRUDIA REKODI YA MWAKA 1980 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top