Dar es Salaam,Tanzania.
YANGA SC imetangaza viingilio vitakavyotumika kushuhudia mchezo
wake wa Kundi A wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe ya Congo DRC unaotarajiwa kuchezwa Jumanne katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akiongea na waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, Jangwani, jijini Dar es Salaam leo,Mkuu wa Idara ya habari na Mawasiliano ya Yanga,
Jerry Muro amesema Yanga imepanga viingilio viwili pekee ambavyo ni Sh. 7000 kwa majukwaa ya
mzunguko na Sh. 30,000 kwa jukwaa Maalumu (VIP).
Aidha mkuu huyo ameongeza kuwa tiketi za mtanange huo unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka nchini zitaanza kuuzwa siku ya Jumatatu.
0 comments:
Post a Comment