Toulouse,Ufaransa.
UBELGIJI imefuzu hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Euro 2016 baada ya Usiku huu kuifunga Hungary kwa mabao 4-0 katika mchezo wa Mtoano uliochezwa katika Uwanja wa Municipal, Toulouse.
Mabao ya Ubelgiji yamefungwa na Toby Alderweireld 10',Michy Batshuayi 78',Eden Hazard 79 ' na Yannick Carrasco 91.
Kwa matokeo hayo sasa Ubelgiji itakutana na Wales katika Robo Fainali.
0 comments:
Post a Comment