Cairo,Misri.
SHILIKISHO la Soka Barani Afrika CAF limetangaza kuiondoka Klabu ya ES Setif ya Algeria katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia vurugu zilizofanywa na mashabiki wake siku ya Jumamosi katika mchezo wa Kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Katika mchezo huo wa Kundi A,wageni Mamelodi Sundowns wakiwa mbele kwa mabao 2-0 ya Tiyiani Mabunda na Khama Billiat,Mwamuzi alilazimika kuuvunja mchezo dakika ya 92 baada ya mashabiki wa ES Setif kuvamia uwanjani na kuanza kufanya vurugu mbalimbali ikiwemo kutupa baruti,mafataki,chupa,mioto hali iliyopelekea baadhi ya mashabiki na wanausalama kujeruhiwa vibaya.
Baada ya kupitia ripoti ya Mwamuzi na Kamisaa wa mchezo ule kamati ya nidhamu ya CAF ikishirikiana na ile ya Mashindano kwa pamoja zimeamua kuiondoa ES Setif katika mashindano ya mwaka huu huku pia ikisubiri adhabu zaidi.
Hii ina maana kwamba sasa Kundi A limebaki na timu tatu za Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini),Zamalek (Misri) na Enyimba (Nigeria)
ES Setif ni Mabingwa mara saba wa Ligi Kuu ya Algeria pia ni Mabingwa wa Afrika mwaka 2014.
0 comments:
Post a Comment