Salalah,Oman
Mshambuliaji nyota wa Tanzania,Elias Maguli amesaini mkataba
wa miaka mitatu wa kuitumikia Klabu ya Dhofar Sports, Cultural, and Social Club inayoshiriki ligi kuu ya nchini Oman akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake katika klabu ya Stand
United ya Shinyanga.
Habari zaidi zinasema Maguli,24,alisaini mkataba huo jana Jumapili baada ya kufikia makubaliano binafsi na viongozi wa Dhofar Sports, Cultural, and Social Club maarufu kama Al-Zaeem , or "The Leader(s)".
Klabu ya Dhofar Sports, Cultural and Sports Club ambayo pia inafahamika kwa jina la utani la Al-Zaeem ( The Leader (s)/The Boss ) ilianzishwa mwaka 1968 ikifahamika kama Al-Shaab kabla ya kubadilishwa jina mwaka 1972
Dhofar SC ambayo iko katika mji wa Salalah SC huutumia uwanja wa Al-Saada Stadium wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 12,000 kwa ajili ya michezo yake ya nyumbani.
0 comments:
Post a Comment