Dar es Salaam,Tanzania.
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, inapenda kuutangazia umma wa Watanzania kuwa hivi sasa tunapokea maombi ya Wafanyabiashara wanaopenda kuwa mawakala wa vifaa vya michezo vya Azam FC.
Hivi karibuni tulifungua duka letu kubwa la kuuza vifaa vya michezo vyenye nembo ya Azam FC 'Azam Sports Shop' lililopo Mtaa wa Mkunguni na Swahili Kariakoo, Dar es Salaam
na pia kufungua huduma maalum kwenye vyombo vya usafiri wa maji vya Azam Marine kwa wasafiri wanaokwenda Unguja Zanzibar kununua vifaa hivyo ndani ya boti.
Kutokana na maombi mengi ya Watanzania waliokuwa nje ya Dar es Salaam kupitia mitandao yetu ya kijamii, wakitaka kuzipata kwa wingi bidhaa zetu mikoani, Azam FC tumeanza kujibu maombi yenu na sasa tunawakaribisha wafanyabiashara watakaopenda kuwa mawakala wetu.
Kwa kuanzia Azam FC tunapenda kuanza na mikoa sita ambayo ni Mbeya, Morogoro,Mwanza, Shinyanga, Kagera na Pwani, hivyo kwa mfanyabiashara yoyote anayependa kushirikiana nasi katika hilo kwenye mikoa hiyo anaombwa kuwasiliana nasi kupitia namba ifuatayo =+255719805868= Na kisha atapewa maelekezo zaidi kwa ajili ya ushirikiano huo wa kubiashara.
Baadhi ya bidhaa rasmi zenye nembo yaAzam FC zilizo na ubora wa hali ya juu, ambazo tayari zimeshaingia sokoni kwa ajili ya kuuzwa ni pamoja na jezi, fulana, taulo, kofia.
Bidhaa nyingine ni skafu, soksi, bendera,makoti ya mvua na track yake, raba za mazoezi, mipira ya mguu,mabegi ya mgongoni yakiwemo ya kuvuta kwa ajili ya safari,Tunawashukuru sana Watanzania na mashabiki wa soka nchini kwa kuendelea kutuunga mkono katika kila jambo tunaloendelea kulifanya tunapenda kutambua mchango wenu na tunawaomba muendelee
hivyo kwa ajili kufikia kilele cha safari yetu ya kuleta mapinduzi katoka soka la Tanzania.
Azam FC; Timu Bora, Bidhaa Bora.
Akhanteni Sana.
Imetolewa na Uongozi wa Azam FC. Juni 24, 2016
0 comments:
Post a Comment