728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, June 21, 2016

    GARETH BALE AVUNJA REKODI YA MIAKA 58 EURO 2016,PIA AIFUKUZIA REKODI YA PLATINI

    Paris,Ufaransa.

    Gareth Bale ameendelea kuwa chachu na moyo wa mafanikio ya Wales katika michuano hiyo mikubwa.

    Baada ya kufunga dhidi ya Slovakia na Uingereza katika mechi zake mbili za awali Euro 2016,mshambuliaji huyo wa Real Madrid alitupia goli lake la tatu katika michuano kikosi cha Chris Coleman kikiifungasha virago Urusi kwa kipigo cha 3-0 katika mechi za kumaliza hatua ya makundi wakimaliza kileleni mwa kundi B Jumatatu.



    Kwa kufanya hivyo, Bale amevunja rekodi ya miaka 58 kwani amempiku Ivor Allchurch kuwa mfungaji wa muda wote wa nchi yake kwenye michuano mikubwa.

    Si Bale pekee aliyeweka historia ya nchi yake lakini mwanzo wake mzuri unamweka katika mtazamo wa kipekee kwenye michuano hiyo. Akifunga katika kila mechi ya hatua ya kundi ni mafanikio yasiyo na ubishi - na hakuna hata mmoja katika michuano miwili iliyopita aliyefanikiwa kufanya hivyo.

    Mwanzo maridadi wa Bale kwenye fainali za 2016 ni jambo ambalo hatujawahi kuona tangu enzi za Milan Baros wa Jamhuri ya Czech na Ruud van Nistelrooy wa Uholanzi waliofunga mechi zote tatu katika Euro 2004.

    Wengine waliowahi kufunga katika michezo mitatu ya makundi ni Michael Platini '84, Stoichkov '96,Allan Shearer '96, Milosevic '00,Milan Baros '04 na Ruud Van Nistelrooy '04.

    Wakati huohuo Bale huenda akaweka rekodi nyingine ya kuwa mchezaji pekee Ulaya kuwahi kupiga mashuti mengi yaliyolenga lango.Mpaka sasa Bale amepiga mashuti 12 langoni katika michezo mitatu nyuma ya Michel Platini aliyepiga mashuti 15 katika fainali zote za mwaka 1984.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: GARETH BALE AVUNJA REKODI YA MIAKA 58 EURO 2016,PIA AIFUKUZIA REKODI YA PLATINI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top