728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, June 30, 2016

    SOUTHGATE AKATAA KUMRITHI ROY HODGSON ENGLAND

    London,England.

    Muda mfupi baada ya Roy Hodgson kujiuzulu kufuatia England kutupwa nje ya michuano ya Euro 2016,Chama cha soka cha nchi hiyo FA kupitia kwa Mtendaji wake Mkuu,Martin Glenn kilitangaza kuwa kingemteua Gareth Southgate kuwa Kocha wa muda wa kikosi hicho lakini taarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba kocha huyo wa zamani wa Middlesbrough amekataa kuchukua kibarua hicho.

    Taarifa zaidi zinasema Southgate,45,ambaye kwasasa ni kocha wa kikosi cha vijana cha England cha Under-21s, amekataa kibarua hicho kwa kile kinachodaiwa kuwa hajavutiwa na mpango wa kuwa Kocha wa muda.

    Taarifa nyingine zinadai Kocha huyo ana hofu na vyombo vya habari vya nchi hiyo kuwa vitampa wakati mgumu kutokana na kutofanya vizuri wakati akiinoa Middlesbrough na kuishusha daraja huku msimu uliopita kikosi chake cha Under 21kikishinda kuonyesha makali katika michuano ya Euro ya vijana na kutolewa mapema.

    Hii ina maana kwamba sasa England inapaswa kufanya kila jitihada kuhakikisha inapata Kocha mpya kabla ya mchezo wake wa kufuzu kombe la dunia la mwaka 2018 dhidi Slovakia hapo Septemba 4 mwaka huu.

    Wakati huohuo taarifa kutoka England zinasema baada ya Southgate kukataa kibarua hicho chama cha soka cha nchi hiyo huenda kikawageukia Makocha Laurent Branc na Glenn Hoddle aliyewahi kukinoa kikosi hicho kutoka mwaka 1996 mpaka 1999.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SOUTHGATE AKATAA KUMRITHI ROY HODGSON ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top