Leceister,England.
Jamie Vardy,29, amezima rasmi habari kuwa anataka kuhamia Arsenal na kuiacha kwenye mataa klabu yake ya Leceister City baada ya kukubali kuingia kandarasi mpya ya miaka minne ya kuendelea kuwachezea wakali hao wa King Power.
Habari hiyo ni pigo kwa Arsenal ambayo wiki mbili zilizopita iliripotiwa kutengua kipengele cha mauzo cha nyota huyo aliyetisha msimu uliopita kwa kupachika mabao makali makali na kuipa Leceister City ubingwa wa kwanza wa Ligi Kuu England baada ya miaka 132 kupita.Arsenal itaka kumnunua kwa paundi milioni 20.
Katika kandarasi hiyo mpya itakayosainiwa baada ya kuisha kwa michuano ya Euro baadae mwezi Julai,Vardy atakuwa akivuna paundi 100,000 kama mshahara wake wa wiki hii ni pungufu ya paundi 20,000 toka katika mshahara wa paundi 120,000 alioahidiwa na Arsenal kama angekubali kutua Emirates.
0 comments:
Post a Comment