Tite
Rio de Janeiro,Brazil.
CHAMA cha soka cha Brazil (CBF) kimemtangaza aliyekuwa kocha wa zamani wa Corinthians, Adenor Leonardo Bacchi maarufu kama Tite" kuwa Kocha Mkuu Mpya timu ya soka ya taifa hilo.
Tite,55,amechukua nafasi ya Carlos Dunga aliyefutwa kazi mapema wiki iliyopita baada ya Brazil/Selecao kutupwa nje ya michuano ya Copa America Centenario.
Changamoto kubwa inayomkabiri Kocha huyo aliyewahi kuvinoa vilabu 13 vya ndani na nje ya Brazil ni kuhakikisha Selecao inafuzu finali za kombe la Dunia za mwaka 2018 nchini Urusi.Kwasasa Brazil iko nafasi ya sita ikiwa imeshinda michezo miwili kati ya sita iliyocheza.
Tite ataanza kukinoa kikosi cha Brazil mara baada ya kuisha kwa michuano ya Olimpiki inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi lake nchini humo kuanzia mwezi Agosti.
Edu Gaspar
Akiwa na kikosi cha Brazil,Tite atakuwa akisaidiwa na Cleber Xavier,Matheus
Bacchi na kiungo wa zamani wa Arsenal ,Edu Gaspar.Hawa wote walikuwa pamoja Corinthians.
Tite anatazamwa kuwa mmoja wa makocha bora nchini Brazil hasa baada ya kuiongoza Corinthians kutwaa mataji sita makubwa katika vipindi viwili tofauti alivyokuwa na miamba hiyo ya Sao Paulo.Baadhi ya mataji hayo ni
Copa Libertadores na Kombe la Dunia la Vilabu.
Wakati huohuo Kocha wa kikosi cha U-20 cha nchi hiyo, Rogerio Micale amepewa jukumu la kuiongoza Brazil kuwania ubingwa wa kwanza wa Olimpiki kwa upande wa soka.
0 comments:
Post a Comment