Paris,Ufaransa.
STAA wa Wales,Gareth Bale,25, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa hatua ya Makundi ya Michuano ya Euro 2016 katika zoezi la upigaji kura lililoendeshwa na mtandao wa Michezo wa Goal.Com.
Ushindi huo umechagizwa na ubora aliouonyesha staa huyo wa Real Madrid ambaye ndiye mchezaji pekee aliyefunga mabao katika michezo yote mitatu ya hatua ya makundi.
Bale amejikusanyia asilimia 27 ya kura zote zilizopita,akifuatiwa na Mlinzi wa Poland,Michal Pazdan aliyejikusanyia asilimia 21.
Pazdan amekuwa muhimili wa Poland kwani ndiyo timu pekee ambayo haijafungwa bao lolote mpaka sasa.
Dimitri Payet ameshika nafasi ya tatu baada ya kupata asilimia 21akiifungia Ufaransa mabao muhimu dhidi ya Romania na Albania na kuisaidia kuibuka kinara wa Kundi A.
Nafasi ya nne imekwenda kwa Andres Iniesta wa Hispania aliyepata asilimia 12.Nafasi ya tano imechukuliwa na nahodha wa Croatia,Darijo Srna aliyepata asilimia 6 ya kura zote.
Nafasi ya sita imeenda kwa Leonardo Bonucci (Italia),Marek Hamsik (Slovakia) na Granit Xhaka (Uswisi) waliojikusanyia asilimia 4
Nafasi ya saba imeenda kwa Michael McGovern (Jamhuri ya Ireland),Alvaro Morata (Hispania) na Jonas Hector (Ujerumani) waliojikusanyia asilimia 1.
0 comments:
Post a Comment