728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 25, 2016

    BINGWA WA COPA AMERICA CENTENARIO KUVAANA NA BINGWA WA EURO 2016


    California,Marekani.

    WAKATI Chile na Argentina zikijiandaa kucheza Fainali siku ya Jumapili ili kumpata bingwa wa Copa America Centenario ,wakuu wa Shirikisho la Soka la Amerika Kusini (CONMEBOL) wamependekeza kuwe na mchezo mmoja wa kuamua nani mbabe kati ya bingwa wa Copa America na yule wa Euro 2016.

    Akiongea jana Ijumaa Rais wa CONMEBOL, Alejandro Dominguez,44, amesema:

    "Tayari tumeshawataarifu wenzetu wa Ulaya (UEFA) juu ya mpango wetu wa kutaka kuwa na mchezo mmoja kati ya bingwa wa Copa America na bingwa wa Euro 2016 ili kujua nani ataibuka mshindi siku hiyo.Tunasubiri jibu lao rasmi,sisi tuko tayari.

    Mbali ya mpango huo,pia Dominguez amesifia mafanikio yaliyofikiwa na michuano ya mwaka huu ya Copa America Centenario ambayo kwa mara ya kwanza katika historia yamefanyika nje ya bara la Amerika Kusini.

    Amesema "Kuna mambo mengi ya kuvutia katika michuano yetu.Tumekuwa na mabao zaidi ya matatu katika kila mchezo.Mashabiki wetu wameonyesha ustaarabu mkubwa.Wamekuwa watulivu kupindukia.Tumekuwa na wastani wa watazamaji 46,000 katika kila mchezo.Hakika haya ni mafanikio makubwa.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BINGWA WA COPA AMERICA CENTENARIO KUVAANA NA BINGWA WA EURO 2016 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top