Nice,Ufaransa.
UBELGIJI imeungana na Italia pamoja na Jamhuri ya Ireland kufuzu hatua ya 16 bora kutoka kundi E baada ya Jumatano usiku kuifunga Sweden kwa bao 1-0 katika mchezo wa mwisho wa makundi uliochezwa katika uwanja wa Allianz Riviera mjini Nice.
Bao pekee la mchezo huo uliokuwa wa mwisho kwa mshambuliaji wa Sweden Zlatan Ibrahimovic anayestaafu limefungwa dakika ya 84 kwa mkwaju mkali na Kiungo Rajda Nainggolan baada ya kupokea pasi safi ya nahodha Eden Hazard toka wingi ya kushoto.
VIKOSI
Sweden : Isaksson, Johansson, Granqvist,Olsson, Forsberg, Ekdal, Kallstrom,Ibrahimovic, Berg, Lindelof
Belgium: Courtois, Meunier,
Alderweireld, Vermaelen, Vertonghen,Witsel, Nainggolan, De Bruyne, Carrasco,Hazard, Lukaku
Katika mchezo mwingine wa kundi E uliochezwa katika uwanja wa Stade Pierre Mauroy,bao la dakika ya 85 la Robbie Brady limeipa Jamhuri ya Ireland ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Italia.
Kwa matokeo hayo Italia,Ubelgiji na Jamhuri ya Ireland zimefanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora huku Sweden ikitupwa nje baada ya kuambulia alama moja katika michezo mitatu.
0 comments:
Post a Comment