Arizona, Marekani.
COLOMBIA wametwaa ushindi wa tatu wa Michuano ya Copa America Centenario baada ya kuwafunga Wenyeji Marekani kwa bao 1-0 katika mchezo Mkali wa kusaka mshindi wa tatu na wa nne uliochezwa Alfajiri ya Leo.
Bao pekee la mchezo huo uliochezwa katika dimba la University of Phonex,Arizona limefungwa dakika ya 31 na mshambuliaji Carlos Bacca baada ya kipa wa Marekani Tim Howard kushindwa kuuwahi mpira wa kichwa uliopigwa na Santiago Arias.
VIKOSI
Marekani: Howard, Orozco (red 90'), Besler, Cameron, Yedlin, Zardes,Bradley (Nagbe 79'), Jones, Bedoya,(Pulisic 74'), Dempsey,Wood
Colombia : Ospina, Fabra, Murillo,Zapata, Arias (red 90'), Torres, Celis (Medina 87'), Cardona, Rodriguez,Cuadrado (Moreno 74'), Bacca (Martinez 79')
Fainali itachezwa kesho kwa Argentina kuvaana na Chile huko East Rutherford, New Jersey.
0 comments:
Post a Comment