Lille, Ufaransa.
MWISHO WA ENZI!!Mshambuliaji wa Kimataifa wa Sweden,Zlatan Ibrahimovic ametangaza kuwa atastaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Sweden mara baada ya kuisha kwa michuano ya Euro 2016.
Akitangaza uamuzi huo jioni ya leo, Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 34,amesema mchezo wa kesho Jumatano wa Kundi E dhidi ya Ubelgiji huenda ukawa mchezo wake wa mwisho kuichezea Sweden ikiwa itapoteza mchezo huo na kushindwa kufuzu hatua ya 16 bora.
Amesema "Mchezo wa mwisho kwa Sweden katika michuano ya Euro utakuwa mchezo wangu wa mwisho kwa Sweden,natumaini haitakuwa kesho".
Hata kama Sweden itafungwa na Ubelgiji na kutupwa nje ya michuano ya Euro,Ibrahimovic amesema hatakuwa na chochote cha kujutia katika maisha yake ya soka.
"Najivunia kuwa nahodha wa Sweden na mafanikio yote niliyoyapata.
Wakati huohuo Ibrahimovic aliyeichezea Sweden michezo 115 na kuifungia mabao 62 pia ametangaza kuwa hataichezea Sweden katika michuano ya Olimpiki mwezi Agosti kama ilivyotangazwa hapo awali.
0 comments:
Post a Comment