Saint Denis,Ufaransa.
ITALIA imetinga Robo Fainali ya Michuano ya Euro 2016 baada ya kuifunga waliokuwa mabingwa watetezi Hispania kwa mabao 2-0 katika Mchezo mkali wa hatua ya 16 Bora uliochezwa Katika Uwanja wa Stade de France,Saint Denis.
Mabao yaliyoipa ushindi Italia katika Mchezo huo yamefungwa dakika za 33 na 91,wafungaji wakiwa ni Giorgio Chiellini na Graziano Pelle.
Kwa matokeo hayo sasa Italia itavaana na Ujerumani katika mchezo wa Robo Fainali unaotarajiwa kuwa wa vuta ni kuvute.
0 comments:
Post a Comment