728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, June 20, 2016

    KWA KAULI HII YA WENGER MASHABIKI ARSENAL MSITARAJIE USAJILI MKUBWA MSIMU HUU,PIA AKIRI KUMKOSA VARDY

    London,England.

    HAKOMI TU!!Kocha wa Arsenal,Mfaransa Arsene Wenger ameendelea kutoa kauli za kukatisha tamaa kwa mashabiki wa klabu hiyo baada ya jana Jumapili kusema kuwa anafikiria kuongeza mchezaji mmoja au wawili pekee katika kikosi chake cha sasa eti kusajili wachezaji wengi kutavuruga mambo.

    Tayari Arsenal imeshamsajili  Granit Xhaka kutoka Borussia Monchengladbach ya Ujerumani kwa ada ya £30m na kumfanya kuwa mchezaji ghari wa tatu nyuma ya Mesut Ozil na Alexis Sanchez.

    Akijibu swali aliloulizwa na mtandao wa Tencent Sports,kuwa ana mpango gani kuhusu ujenzi mpya wa kikosi chake katika kipindi hiki cha usajili.
     
    Wenger amesema "Tayari tumeshanunua mchezaji mmoja, Granit Xhaka kutoka Monchengladbach.
    Tumepoteza wachezaji Watatu.Tumewapoteza [Mikel] Arteta, [Tomas] Rosicky na [Mathieu] Flamini.

    Tumemnunua Kiungo mmoja na bado tupo sokoni tunaangalia uwezekano wa kununua mchezaji mmoja au wawili zaidi.”

    Wenger ameongeza “Lakini siyo rahisi.Siyo suala la kununua tu.Pia tunapaswa tubakishe uwiano
    mzuri. Ukinunua Wachezaji wengi zaidi unaharibu uwiano katika kikosi chako.Hivyo wachezaji watatu ndiyo idadi ya juu kabisa tutakayoweza kununua”

    Wakati huo huo Arsene Wenger amekiri kuwa mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Leceister City,Muingereza Jamie Vardy,29,umekufa baada ya mchezaji huyo mpaka sasa kushindwa kuonyesha nia ya kutaka kuondoka King Power Stadium na kutua Emirates.
    "Kwasasa Vardy ni mchezaji wa Leceister City na kwa jinsi hali ilivyo nadhani atabaki hapo".Alimaliza Wenger ambaye msimu uliopita alisajili wachezaji wawili pekee,Peter Cech kutoka Chelsea na Mohammed Elneny kutoka FC Basel.

    Kauli hizo mbili zimekuwa ni kinyume cha matarajio ya mashabiki wa Arsenal ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitamani kuiona timu yao ikifanya usajili mkubwa na hatimaye kutwaa mataji makubwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KWA KAULI HII YA WENGER MASHABIKI ARSENAL MSITARAJIE USAJILI MKUBWA MSIMU HUU,PIA AKIRI KUMKOSA VARDY Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top