London,England.
Kocha Jose Mourinho ameweka wazi nia yake ya kufundisha soka kwa mara nyingine hasa nchini England lakini amesisitiza kuwa bao hajasaini mkataba na klabu yoyote ile ikiwemo Manchester United.
Mourinho,53,ametoka kauli hiyo jana jumamosi alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha Sky Sports katika ukumbi wa 02 Arena alipokwenda kutazama pambano la masumbwi la Antony Joshua na Prince Martin.
Amesema "Kwa sasa naweza kuahidi kuwa bao sijasaini mkataba na klabu yoyote ile.Niko katika nafasi ya kupokea ofa toka katika klabu yoyote,taifa lolote lakini zaidi ningependa kufundika klabu kuliko timu ya taifa.
Wakati huohuo Jose Mourinho amekiri kukataa ofa ya kufundisha soka nchini Syria baada ya maofisa wa chama cha soka nchi hiyo kumtaka aisaidie Syria kufuzu michuano ya kombe la dunia la mwaka 2018 huko Urusi.
0 comments:
Post a Comment