728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, April 16, 2016

    HIZI HAPA HABARI 8 ZA USAJILI BARANI ULAYA JUMAMOSI YA LEO

    Ilkay Gundogan

    Griezmann: Paris Saint-Germain imeripotiwa kuanza kujiandaa na maisha bila ya nyota wake Zlatan Ibrahimovic baada ya kudaiwa kuanza mazungumzo ya kuwasajili Antoine Griezmann wa Atletico Madrid na Marco Reus wa Borussia Dortmund.(TF1)

    Gundogan:Man City wameripotiwa kushinda mbio za kumuwania kiungo Ilkay Gundogan baada ya ofa yake ya £30m kukubaliwa na Borussia Dortmund.Taarifa rasmi itatolewa mwisho wa msimu.(The Sun)

    Sadiq:Arsenal imepata upinzani katika mbio zake za kutaka kumnasa kinda wa AS Roma Umar Sadiq,19 mwenye thamani ya £10m baada ya vilabu vya Tottenham na Liverpool navyo kuripotiwa kumtaka nyota huyo wa Nigeria ambaye kiuchezaji anafananishwa na Nwankwo Kanu.(La Gazzetta Dello Sport)

    Babacar: Liverpool wana matumaini makubwa ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Fiorentina Msenegal Khouma Babacar,23.Babacar ameifungia Fiorentina mabao matano katika michezo 18 ya Seria A.(Calciomercato)

    Burkart:Manchester United wamefikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji kinda wa FC Zurich Nishan Burkart,16.(Bilk)

    Sessegnon:Vilabu vya Arsenal na Liverpool vimeripotiwa kuingia katika vita ya kutaka kumsajili mlinzi wa kushoto wa Fulham Ryan Sessegnon,15. 

    Gimenez:Matumaini ya Chelsea kumnasa mlinzi wa Atletico Madrid  Jose Gimenez yameingia mdudu baada ya vilabu vya  Barcelona na Real Madrid kuripotiwa kuandaa kitita cha £50m ili kumsajili.(Mundo Deportivo)

    Ranieri:Claudio Ranieri amesema haitaji kujengewa mnara wa kumbukumbu kwa sasa hata kama Leicester City itatwaa ubingwa wa ligi kuu.(Daily Star)



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI 8 ZA USAJILI BARANI ULAYA JUMAMOSI YA LEO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top