London,England.
AMETIBUA!!Kurejea uwanjani kwa nyota wa Manchester United Wayne Rooney kumemfanya kocha Roy Hodgson kuwaengua nyota wa Arsenal Theo Walcott na Alex Oxlade-Chamberlain katika kikosi cha England kitakachokwenda kushiriki katika kinyang'anyiro cha kombe la mataifa ya Ulaya (Euro 2016) huko Ufaransa mwezi Juni mwaka huu.
Kwa mujibu wa gazeti la The Daily Mirror ni kuwa Hodgson ameamua kuwa atamtumia Wayne Rooney,31 katika nafasi ya winga ya kulia badala ya ushambuliaji kama ilivyozoeleka.
Katika nafasi ya ushambuliaji Hodgson atawatumia nyota wawili wa Tottenham Harry Kane na Dele Alli huku Danny Welbeck akitumika kama winga wa kushoto.
Winga ya kulia ambayo ndiyo kimbilio la Walcott na Alex Oxlade-Chamberlain huku kutakuwa na nahodha Wayne Rooney,Jamie Vardy na Raheem Sterling.
Hivyo basi hii ina maana kuwa Theo Walcott na Alex Oxlade-Chamberlain hawatakuwa na chao/nafasi katika mshindano ya mwaka huu ya mataifa ya Ulaya.
Taarifa za ndani zinasema Roy Hodgson amelazika kumchukua Wayne Rooney kutokana na kuwa na uzoefu mkubwa katika michuano ya kimataifa.Ikumbukwe pia nyota huyo wa Manchester United ndiye anayeshikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa England baada ya kuvunja rekodi ya Sir Bobby Charlton.
0 comments:
Post a Comment