728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, April 30, 2016

    YANGA YAICHAPA TOTO AFRICANS 2-1 CCM KIRUMBA

    Mwanza,Tanzania.

    Mabao mawili ya kipindi cha pili yameipa Yanga SC ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Toto Africans katika mchezo mkali wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliopigwa katika Uwanja wa CCM Kirumba,Mwanza.

    Toto Africans ndio walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa William Kimanzi aliyefunga kwa kichwa dakika ya 39 ya kipindi cha kwanza akiunganisha kona ya Abdalah Seseme.

    Kipindi cha pili Yanga SC iliuanza mchezo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Hamis Tambwe.Tambwe alifunga bao hilo kwa kichwa na kufikisha mabao 19 akitumia vyema krosi ya Donald Ngoma.

    Dakika ya 77 mlinzi wa kulia Juma Abdul aliifungia Yanga SC bao la ushindi kwa shuti kali akimalizia mpira uliotemwa na mlinda mlango wa Toto Africans Mussa Mohammed

    Kufuatia ushindi huo Yanga SC imefikisha pointi 65 baada ya kucheza michezo 25,Azam FC iko nafasi ya pili ikiwa na pointi zake 58 nafasi ya tatu imekaliwa na Simba SC yenye pointi 57.

    Katika mchezo mwingine African Sports imeichapa Coastal Union kwa bao 1-0 katika mchezo mkali uliopigwa katika uwanja wa CCM Mkwakwani,Tanga.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: YANGA YAICHAPA TOTO AFRICANS 2-1 CCM KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top