London,England.
Tottenham imeendelea kuipa preshaLeiceister City katika mbio za kuusaka ubingwa wa ligi kuu England baada ya jumatatu usiku kuinyuka Stoke City mabao 4-0 huko Britannia na kufanya tofauti ya pointi kuwa tano.
Tottenham inayosaka ubingwa wake wa kwanza wa England tangu mwaka 1961 imepata ushindi huo mkubwa ugenini kwa mabao ya Harry Kane na Dele Alli.
Harry Kane ndiye aliyekuwa wa kwanza kuliona lango la Stoke baada ya kufunga bao dakika ya 10 tu ya mchezo akimalizia pasi ya Moussa Dembele.Dakika ya 67 Dele Alli aliifungia Tottenham bao la pili kwa pasi ya Christian Eriksen.
Harry Kane aliiongeza bao la tatu dakika ya 71 kabla ya Alli kufunga bao la nne dakika ya 82 akiunganisha pasi ya Christian Eriksen
Kufuatia matokeo hayo Tottenham imefikisha pointi 68 ikiwa nafasi ya pili nyuma ya vinara Leceister City wenye pointi 73
0 comments:
Post a Comment