728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, April 19, 2016

    MAPHARAO WA MISRI WAANZA MAPEMA MIPANGO YA KUIVAA STARS AFCON

    Cairo,Misri.

    Misri imetangaza kuwa itacheza mchezo mmoja wa kimataifa wa kirafiki na Malawi kabla ya kuivaa Taifa Stars katika mchezo wa marudiano wa kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya AFCON. 

    Mchezo huo ambao unaenda sambamba na kalenda ya FIFA umepangwa kuchezwa Aprili 30 katika uwanja ambao bado haujatajwa.

    Mara ya mwisho kwa timu hizo kukutana ilikuwa ni mwaka 2008 ambapo Malawi wakiwa nyumbani Blantyre waliifunga Misri bao 1-0 kupitia kwa chiukepo Msowoya.

    Misri iko kileleni mwa kundi G ikiwa na pointi zake 7 hivyo ushindi wowote ama sare dhidi ya Taifa Stars Uwanja wa Taifa vitaipa nchi hiyo ya Afrika Kaskazini tiketi ya kushiriki michuano ya AFCON hapo mwakani nchini Gabon.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAPHARAO WA MISRI WAANZA MAPEMA MIPANGO YA KUIVAA STARS AFCON Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top