Ramadan Sobhy
Cairo,Misri.
Ama kweli kila shetani na mbuyu wake!!We ukipenda hiki mwenzio anapenda kile na hivi ndiyo maisha yalivyo.
Wakati Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wakitajwa kuwavutia watu wengi,nyota wa Al Ahly Ramadan Sobhy yeye yuko tofauti na wala havutiwi kabisa na wababe hao wa La Liga.
Akijibu swali aliloulizwa katika runinga ya CBC ya nyumbani kwao Misri lililouliza kati ya Messi na Ronaldo ni yupi anayemvutia zaidi,Sobhy amedai anavutiwa na winga wa Paris Saint-
Germain Mbrazil Lucas Moura.
Amesema “[Lionel] Messi na [Cristiano] Ronaldo siyo wachezaji wangu kipenzi licha ya kwamba wamefanya mengi katika soka,navutiwa zaidi na Lucas Moura.
Swali la pili“Je,wewe ni shabiki wa timu gani Ulaya? Mi ni shabiki wa kutupwa wa Real Madrid na naitakia kheri katika michezo yake ya nusu fainali ya Ulaya dhidi ya Manchester City.
Licha ya kwamba Sobhy amekiri kwamba yeye ni shabiki wa kutupwa wa Real Madrid lakini amesema akipata nafasi ya kucheza soka Ulaya atapenda zaidi kucheza Arsenal anakocheza raia mwenzie wa Misri Mohamed Elneny.
Siku za hivi karibuni Sobhy amekuwa lulu sana hasa baada ya kuifungia Misri bao la ushindi dhidi ya Nigeria katika kinyang'anyiro cha kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya AFCON 2017 huko Gabon.
0 comments:
Post a Comment