Vilabu vya Yanga na Azam FC leo jioni vitashuka dimbani kucheza michezo zao za viporo vya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Yanga itakuwa Uwanja wa Taifa kuikaribisha Mgambo JKT kutoka Tanga huku Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati Azam FC wao watakuwa katika dimba lao la nyumbani la Azam Complex,Chamazi kuwaalika Wanalizombe Majimaji kutoka Songea.
Ikiwa Yanga na Azam FC zitashinda michezo yao ya leo jioni zitakuwa zimeishusha Simba SC mpaka nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mpaka sasa Yanga iko kileleni na pointi zake 59,ikifuatiwa na Simba SC yenye pointi 57 huku Azam FC ikiwa ya tatu za pointi zake 55.
Ligi hiyo itaendelea tena Jumamosi Aprili 30, 2016,Ratiba itakuwa hivi:
Toto Africans Vs Yanga SC
African Sports Vs Coastal Union
Mwadui FC Vs Stand United
Mtibwa Sugar Vs Mbeya City
Prisons Vs JKT Ruvu
0 comments:
Post a Comment