Rafinha
Na.sokaextra.blogspot.com
Rafinha:Arsenal imeahidi kumpa mkataba wa miaka mitatu mlinzi wa kulia wa Bayern Munich Mbrazil Márcio Rafael Ferreira de Souza (Rafinha),30 ikiwa atakubali kujiunga nayo mwishoni mwa msimu huu.Arsenal inamuona Rafinha kama mtu sahihi wa kumpa changamoto mlinzi wake kinda Hector Bellerin.(Bild)
Depay:Manchester United wameripotiwa kutaka kumpeleka Southampton winga wake Memphis Depay kama mpango wa kuishawishi klabu hiyo ya St.Marys ikubali kumuachia winga wake hatari Msenegal Sadio Mane.(Daily Star)
Silva:Mlinzi kisiki wa Paris Saint-Germain Mbrazil Thiago Silva anataka kujiunga na Barcelona msimu ujao ili aweze kushinda taji la ligi ya mabingwa barani Ulaya.( Mundo Deportivo)
Skrtel:Besiktas imefanya mazungumzo na mlinzi wa Liverpool Martin Skrtel juu ya uwezekano wa kumsajili katika kipindi kijacho cha majira ya kiangazi.(Fanatik)
De Gea:Real Madrid itajaribu tena kutaka kumsajili mlinda mlango David De Gea ikiwa klabu yake ya Manchester United itashindwa kupata nafasi ya kucheza michuano ya klabu bingwa Ulaya.(Marca)
Dzeko:Roma imepanga kumpiga bei mshambuliaji wake Edin Dzeko,30 baada kushindwa kuwika msimu huu.Kwa mujibu wa mkurugenzi wa michezo Walter Sabatini ni kwamba Roma itamuuza nyota huyo wa zamani wa Manchester City kati ya England au Ujerumani.(Sport.ba)
Rahman:Fenerbahce imeripotiwa kutaka kumsajili mlinzi wa kushoto wa Chelsea Mghana Baba Rahiman ili kuziba nafasi ya mlinzi wake kinda Caner Erkin,21 anayetarajiwa kuhama mwishoni mwa msimu huu.(Fanatik)
Walcott:AC Milan inataka kumpeleka San Siro winga wa Arsenal Muingereza Theo na imeripotiwa kuwa inataka kumtumia kinda wake Manuel Locatelli katika kurahisisha dili hilo.(CalcioMercatoWeb)
0 comments:
Post a Comment