Berlin,Ujerumani.
Borussia Dortmund itavaana na Bayern Munich katika mchezo wa fainali wa kombe la ligi maarufu kama DFB-Pokal Mei 21 baada ya Jumatano usiku kuichapa Hertha Berlin 3-0 katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa huko Olympic Stadium.
Mabao yaliyoipeleka Borussia Dortmund katika fainali ya tatu ndani ya miaka mitano yamefungwa na Gonzalo Castro (20), Marco Reus (75) na Henrikh
Mkhitaryan (83).
Bayer Munich ambao ni mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo baada ya kutwaa ubingwa mara 17 wao wametinga fainali baada ya Jumanne usiku kuichapa Werder Bremen 2-0.
0 comments:
Post a Comment