Ndola,Zambia.
Mabingwa wa Zambia Zesco United wamekuwa wa kwanza kutinga hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa Afrika baada ya jioni ya leo kuichapa Stade Malien ya Mali kwa mabao 2-1huko katika dimba la Mwanawasa,Ndola.
Mabao ya Zesco United yamefungwa dakika za 5 na 82 na Jesse Jackson
Were na Maybin Mwaba huku Stade Malien wao wakipata bao la kufutia machozi dakika ya 58 kupitia kwa Moussa Coulibaly.
Kwa matokeo hayo Zesco United imefanikiwa kuitupa nje ya michuano hiyo Stade Malien kwa jumla ya mabao 5-2 baada ya mchezo wa kwanza kushinda kwa mabao 3-1.
0 comments:
Post a Comment