Milan,Italia.
MAISHA ni safari ndefu sana tena yenye kila aina ya matukio.Kila mmoja wetu katika dunia hii ana kitu cha kusimulia.Kiwe kibaya au kizuri ana kitu cha kusimulia.
Kiungo wa Inter Milan Mbrazil Felipe Melo de Carvalho amefichua kuwa kama siyo kucheza soka basi leo hii angekuwa muuaji.
Akiongea na Sky Italia Melo,32 anaamini mambo yangekuwa tofauti sana kama asingekuwa mcheza soka.
Melo ambaye amezaliwa na kukulia huko Volta Redonda,Brazil eneo linalosifika kwa uhalifu,uuzaji wa madawa ya kulevya,wizi na uporaji wa kutumia silaha amesema,
"Maisha yetu yalikuwa magumu sana.Yalijaa umasikini mkubwa.Baba alilazimika kufanya kazi shifti mbili kwa siku ili aweze kupata pesa ya kutununulia chakula na mahitaji mengine.
Nimepitia shida nyingi sana naamini ndizo zimenifanya nitimize ndoto zangu. Nilikuwa na marafiki wabaya,wezi na wauaji kama siyo soka leo hii ningekuwa mmoja wao.
Kuna siku nilikwenda mazoezini na niliporudi nyumbani nilikuta rafiki yangu ameuwawa.Ilinibidi kuchagua moja kati ya kucheza soka ama kuwa mharifu.
Nashukuru niliweza kuepuka uharifu na kuchagua kucheza soka na kuwa na maisha tofauti".Alimaliza Melo aliyewahi kuchezea pia vilabu vya Fiorentina, Juventus, Galatasaray.
0 comments:
Post a Comment