Kinshansa,Congo.
Upinzani katika ya vilabu vya TP Mazembe na AS Vita Club umechukua sura mpya baada ya siku ya Jumatano basi lililokuwa limewabeba wachezaji wa TP Mazembe kushambuliwa kwa mawe huko Kinshasa.
TP Mazembe wamekutwa na tukio hilo wakati wakirejea nyumbani Lubumbashi, wakitoka katika mchezo wa ugenini wa ligi ya Congo dhidi ya AS Vita Club huko Stade Des Martrys, Kinshasa
Katika tukio hilo Kiungo wa Kimataifa wa Zambia Rainford Kalaba alijeruhiwa vibaya kichwani baada kupondwa na jiwe na watu wanaoaminika kuwa ni mashabiki wa AS Vita Club.
Mchezo huo uliisha kwa sare ya bila kufungana huku timu zote zikimaliza na wachezaji pungufu.
Bernard Morrison wa Vita Club alikuwa wa kwanza kutolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumchezea rafu mbaya mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania Thomas Ulimwengu.
Dakika chache baadae Salif Coulibaly wa TP Mazembe nae alitolewa nje ya uwanja baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa mchezo mbaya.
AS Vita na TP Mazembe zote zinaongoza ligi zikiwa zimefikisha pointi 11 kila moja.
0 comments:
Post a Comment