London,England.
YAMETIMIA!!Chelsea imekubali kutoa ada ya £28m ili kumsajili kiungo wa AS Roma Mbelgiji Radja Nainggolan,27 hii ni kwa mujibu wa mtandao wa The Mirror .
Chelsea imekubali kutoa kitita hicho baada ya mabosi wa AS Roma kuridhia kupunguza bei toka £31m mpaka £28m kufuatia kuwa katika mazungumzo ya kina ya takribani saa 48.
Nainggolan aliyewahi kukipiga na Cagliari anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne na nusu wa kuitumikia Chelsea hii ni baada ya kocha Antonio Conte kumuweka katika orodha ya nyota anaowataka Stamford Blidge.
Msimu huu Nainggolan ameichezea AS Roma jumla ya michezo 39 na kufanikiwa kupachika mabao matano.
0 comments:
Post a Comment