Barcelona,Hispania.
Baada ya mvutano wa muda mrefu hatimaye Barcelona imetangaza kumruhusu nyota wake Neymar kuichezea Brazil katika michuano ya Olympiki inayotarajiwa kufanyika nchini humo baadae mwaka huu.
Barcelona imekubali kumuachia Neymar,24 baada ya kufanya majadiliano marefu na chama cha soka cha Brazil chini ya Rais wake Marco Polo del Nero.
Pia katika majadiliano Barcelona na Brazil zimekubaliana kuwa nyota huyo wa zamani wa Santos hatajumuiwishwa katika kikosi cha Brazil kitakachokwenda Marekani mwezi Juni kushiriki michuano ya Copa America Centenario licha ya Neymar mwenyewe kusema kuwa angependa kuwemo katika michuano yote miwili.
Sababu kubwa iliyotolewa na Barcelona kuomba Neymar asijumuishwe katika michuano ya Copa America Centenario imedaiwa kuwa ni kumuepusha na majeruhi pamoja na uchovu.
Michuano ya Olympiki inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake kuanzia Agosti 3-21 nchini Brazil huku wenyeji Brazil wakipania kutwaa taji la michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu lilipoasisiwa miaka mingi iliyopita.
Brazil iko kundi A pamoja na mataifa ya Afrika Kusini,
Iraq na Denmark na mchezo wake wa kwanza utakuwa Agosti 4 dhidi ya Afrika Kusini huko Brasilia.
0 comments:
Post a Comment