Cairo,Misri.
Kocha mkuu wa Al Ahly Mholanzi Martin Jol ametangaza kikosi cha wachezaji 19 kutakachoshuka dimbani leo huko jijini Alexandria kuivaa Yanga katika mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya 16 bora ya michuano ya vilabu bingwa Afrika.
Aidha katika kikosi hicho Jol amewatema wachezaji sita ambao ni Saleh Gomaa, Ahmed El-Sheikh na John Antwi,Bassem Ali,Mohamed Naguib na Ahmed Hamdy.Wachezaji hao sita wameondolewa kwa sababu za kiufundi.
Wakati huohuo Al Ahly itaendelea kumkosa kipa wake Ahmed Adel Abdel-
Moneim anayesumbuliwa na majeruhi.
Kikosi kamili cha Al Ahly ni:
Makipa: Sherif Ekramy na Mosaad Awad.
Mabeki: Saad Samir, Rami Rabia, Ahmed Hegazy, Hussein El-Sayed, Ahmed Fathi,Mohamed Hany na Sabry Rahil.
Viungo: Hossam Ghaly, Hossam Ahsour, Abdallah El-Said, Mo’men Zakaria,
Walid Soliman, Ramadan Sobhy na Amr El-Sulaya.
Washambuliaji: Amr Gamal, Malick Evouna na Emad Meteb.
Katika mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa saa 2:30 kwa majira ya saa za Afrika Mashariki Al Ahly inahitaji sare ya bila kufungana ama ushindi wowote ule ili iweze kutinga hatua ya makundi.Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Dar es salaam timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1.
0 comments:
Post a Comment