London,England.
Zingua Tukuzingue!!Kiwango kibovu alichokionyesha Emmanuel Emenike,28 katika mchezo wa ligi kuu England ulioisha kwa Westham kulazimishwa sare ya 2-2 Leicester City Jumamosi iliyopita kimewachukiza mashabiki wa Westham hata kufikia hatua ya kumtaka kocha mkuu wa timu hiyo Mcroatia Slaven Bilic amtimue mshambuliaji huyo toka Nigeria.
Mashabiki hao wakitumia mtandao wa kijamii wa Twitter wamemponda mfungaji huyo bora wa AFCON 2013 kwa kushindwa kupiga hata shuti moja golini licha ya kucheza kwa dakika zote 90 katika mchezo huo ambao Westham ilihitaji ushindi ili ifufue matumaini ya kuingia top four.
Baadhi ya maoni ya mashabiki hapo kupitia mtandao wa Twitter yalikuwa hivi.
Jack Loft "Bila shaka Emenike ndiye mchezaji mbovu zaidi kumuona akiichezea West Ham.”
Phil Mead,“Emenike anapaswa kuondoshwa.Mchezaji gani huyu aliyeslow (taratibu) kama Kobe!!
Sam Clack "Siwezi kwenda uwanjani tena kumtazama Emenike akicheza.
Hata hivyo kocha Slaven Bilic amemtetea Emenike na kusema aliamua kumsajili mshambuliaji huyo kutokana na kuwa na uwezo mzuri akisisitiza kabla ya kumleta Westham alishawahi kufanya nae kazi Urusi na Uturuki.
Emenike alijiunga na Westham kwa mkopo mwezi Januari mwaka huu akitokea Fenerbahce ya Uturuki huku kukiwa na kipengele cha kumsajili moja kwa moja.Mpaka sasa Emenike ameifungia Westham mabao matatu katika michezo 12 ya ligi kuu.
0 comments:
Post a Comment