Turin,Italia.
Timu ya taifa ya Italia imepata pigo baada ya kiungo wake tegemeo Claudio Marchisio kuripotiwa kuwa atakosa michuano ijayo ya Ulaya maarufu kama Euro baada ya jana jumapili kuumia goti wakati akiichezea klabu yake ya Juventus katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Palermo.
Marchisio,30 alilazimika kutolewa uwanjani dakika ya 16 tu ya mchezo na nafasi yake kuchukuliwa na Mario Lemina baada ya kugongana na kiungo wa Palermo Franco Vazquez.
Taarifa kutoka katika mtandao rasmi wa klabu ya Juventus zinasema Marchisio aliyeichezea Italia jumla ya michezo 54 anatarajiwa kufanyiwa upasuaji ndani ya siku chache zijazo hivyo atakuwa nje ya dimba kwa kipindi kirefu hali itakayopelekea pia akose michuano ya Euro 2016 itakayopigwa nchini Ufaransa kuanzia mwezi Juni.
0 comments:
Post a Comment