Dar es salaam,Tanzania.
Ligi Kuu ya Bara inatarajiwa kuendelea leo jumamosi kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, huku kila timu ikisaka ushindi katika michezo hiyo ili kujiweka katika mazingira mazuri kwenye msimamo wa ligi.
Jumamosi, Young Africans watakua wenyeji wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku Ndanda FC wakiwakaribisha wakata
miwa wa Kagera Sugar katika uwanja wa Nang’wanda Sijaona mjini Mtwara.
Coastal Union watawakaribisha maafande wa JKT Ruvu katika uwanja
wa Mkwakwani jinini Tanga.
Jumapili, Simba SC watacheza na Toto Africans katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment