Munich,Ujerumani.
Klabu ya VFL Wolfsburg ya Ujerumani imetangaza kumtupia virago aliyekuwa mshambuliaji wake Mdenmark Nicklas Bendtner.
Akiripoti uamuzi huo mzito Mkurugenzi wa michezo wa VFL Wolfsburg Klaus Allofs amesema Bendtner,28 ametupiwa virago baada ya kuwa na matatizo na klabu kwa kipindi kirefu sasa hali iliyopelekea nyota huyo wa zamani wa Arsenal aondolewe kikosini na kulazimishwa kufanya mazoezi peke yake.
Allofs ameongeza kuwa kwa kipindi kirefu kumekuwa na mazungumzo kati ya klabu na mchezaji huyo ili kuweka sawa hali ya mambo lakini baada ya kuona suluhu haipatikani leo VFL Wolfsburg imetangaza kuvunja mkataba na Bendtner.Mkataba huo ulitarajiwa kuisha mwaka 2017.
Bendtner alijiunga na VFL Wolfsburg mwaka 2014 kwa uhamisho huru akitokea Arsenal.Mpaka anatupiwa virago Bendtner ameichezea VFL Wolfsburg michezo 47 na kuifungia mabao tisa.
0 comments:
Post a Comment