728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, April 23, 2016

    BAADA YA KUITOA YANGA,AL AHLY SASA KUJIPIMA UBAVU KWA AS ROMA YA ITALIA

    Cairo,Misri.

    Mabingwa wa Misri Al Ahly SC ambao majuzi wameitupa Yanga nje ya michuano ya klabu bingwa ya Afrika wametangaza kufikia makubaliano ya kucheza mchezo mmoja wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya AS Roma ya Italia.

    Al Ahly inataka kuutumia mchezo huo utakaopigwa katika nchi za Falme za Kiarabu kwa ajili ya kujiweka fiti na michezo ya makundi ya klabu bingwa ya Afrika. 

    Hii itakuwa ni mara ya tatu kwa Al Ahly kupimana ubavu na AS Roma.Katika mchezo wa kwanza uliopigwa mwaka 2002 huko Misri,Al Ahly ilishinda 2-1 kwa mabao ya Ibrahim Said na Evelino huku Vicenzo Montella akiifungia AS Roma bao la kufutia machozi.

    Katika mchezo wa pili uliopigwa mwaka 2008 Al Ahly ilichapwa 3-0 na Roma kwa mabao ya Mauro Esposito,Matteo Brighi na David Pizarro.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BAADA YA KUITOA YANGA,AL AHLY SASA KUJIPIMA UBAVU KWA AS ROMA YA ITALIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top