728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, April 30, 2016

    MECHI ZA LIGI BARA KUENDELEA LEO,KESHO RATIBA NZIMA IKO HAPA

    Dar es salaam,Tanzania.

    Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendeleo wikendi hii kwa michezo sita kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini.

    Jumamosi mabingwa wanaotetea taji hilo, Yanga ya Dar es Salaam itakuwa mgeni wa Toto Africa katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa CCM-Kirumba jijini Mwanza huku Coastal Union ikipambana na African Sports kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

    Mechi nyingine zitakuwa ni kati ya Mwadui FC watakaokuwa wenyeji wa
    Stand United kwenye Uwanja wa Mwadui,Shinyanga wakati Mbeya City watakuwa wageni wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu,Mvomero mkoani Morogoro na katika Dimba la Sokoine jijiji Mbeya Tanzania Prisons itaumana na JKT Ruvu katika mfululizo wa mechi za ligi hiyo.

    Jumapili Simba itaikaribisha Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa,Dar es Salaam.

    Michezo yote itaanza saa 10.000 jioni na kurushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni ya Azam.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MECHI ZA LIGI BARA KUENDELEA LEO,KESHO RATIBA NZIMA IKO HAPA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top