728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, April 27, 2016

    ENYEAMA AITOA KIMASOMASO AFRIKA

    Lagos,Nigeria.

    Mlinda mlango Mnigeria Vincent Enyeama anayedakia Lille ya Ufaransa ametajwa na kitengo cha CIES Football Observatory cha Uswisi katika orodha ya walinda mlango 10 waliofanya vizuri msimu huu katika ligi kubwa za Ulaya.

    CIES imetoa orodha hiyo kwa kuzingatia idadi ya magoli ya kufungwa katika mchezo mmoja,idadi ya dakika kwa goli,idadi ya pasi katika mchezo mmoja,idadi ya kuokoa michomo (saves) kwa mchezo mmoja na wastani wa jumla wa kuokoa michomo.

    Katika orodha hiyo Enyeama,33 yuko nafasi ya sita nyuma ya Manuel Neuer (Bayern Munich), Jan
    Oblak ( Atletico Madrid), Gianluigi Buffon ( Juventus), Kevin Trapp ( PSG) na Claudio Bravo ( Barcelona).

    Walinda mlango waliopigwa bao na Enyeama ni Hugo Lloris (Tottenham), Alphonse Areola (Villarea)l, Keylor Navas ( Real Madrid) na Pepe Reina ( Napoli).

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ENYEAMA AITOA KIMASOMASO AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top