Schmeichel:Barcelona imeripotiwa kuandaa kitita cha £15m kwa lengo la kumsajili mlinda mlango wa Leicester City Mdenmark Kasper Schmeichel ili kuchukua nafasi ya mlinda mlango wake Marc-Andre ter Stegen anayetaka kuondoka klabuni hapo. (The Sun)
Depay:Kocha mkuu wa Manchester United Mholanzi Louis Van Gaal amewaambia mabosi wa klabu hiyo kumpiga bei winga Memphis Depay.Van Gaal amefikia uwamuzi huo baada ya Depay,22 kushindwa kuonyesha kiwango cha kuridhia tangu atue Old Trafford kwa dau la £25m akitokea PSV Eindhoven.(Sunday Mirror)
Burke:Arsenal imeripotiwa kumfukuzia winga kinda wa Nottingham Forest Mscotland Oliver Burke ili kuchukua nafasi ya Alex Oxlade Chamberlain anayetarajiwa kuuzwa mwishoni mwa msimu.Burke,19 ameifungia Nottingham Forest mabao mawili katika michezo 19.(The Sun)
Gomes:Juventus imeripotiwa kubakiza masuala madogo madogo kabla ya kutangaza kukamilisha usajili wa kiungo fundi wa Valencia Mreno Andre Gomes.Gomes anayedaiwa kuwa na thamani ya €30m anakuja kuziba pengo la Claudio Marchisio aliye nje ya dimba akiuguza jeraha la goti.(Gazzetta World)
Song:Crystal Palace imesema iko tayari kumsajili kiungo wa FC Barcelona Mcameroon Alex Song ikiwa tu nyota huyo wa zamani wa Arsenal atakubali kushusha mshahara wake wa £80,000 kwa wiki (The Sun)
Quina:West Ham imeshinda mbio za kumsajili kiungo wa Chelsea Domingos Quina, baada ya kuizidi ujanja Arsenal ambayo awali ililipotiwa kukaribia kumsainisha mkataba nyota huyo mwenye miaka 17.Quina anatarajiwa kumwaga wino wa kuichezea Westham leo mchana.(Daily Mirror)
Lacazette:Tottenham imedaiwa kuongoza katika mbio za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Lyon Mfaransa Alexandre Lacazette lakini inakabiriwa na upinzani mkali toka vilabu vya Manchester United,Everton na Liverpool ambavyo navyo vimeripotiwa kumfukuzia nyota huyo mwenye thamani ya £23.5m.(Daily Mirror)
Vlahovic:Vilabu vya Arsenal na Juventus vimedaiwa kuwa katika vita kali ya kumuwania mshambuliaji kinda wa Partizan Belgrade Dusan Vlahovic,16.(Daily Mirror)
Howe :Kocha wa Bournemouth Eddie Howe ameripotiwa kuwa chaguo la kwanza la Everton kuchukua nafasi ya kocha Roberto Martinez anayetarajiwa kufutwa kazi mwishoni mwa msimu huu.(The Sun)
Ben Arfa:Chelsea imeungana na Liverpool na Paris Saint-Germain katika mbio za kuiwaniA saini ya winga wa Nice Mfaransa Hatem Ben Arfa.Ben Arfa,29 atakuwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu.(talkSPORT)
Ounas:Manchester United imeripotiwa kuwa karibu kumsajili mshambuliaji wa Bordeaux Adma Ounas,19 licha ya kukabiriwa na upinzani mkali toka kwa Monaco.(le10sport.com)
Stones:Kocha ajaye katika klabu ya Chelsea Muitaliano Antonio Conte amesema hana mpango wa kumsajili mlinzi wa kati wa Everton John Stones licha ya kwamba nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 kutakiwa na makocha waliomtangulia.(The London Evening Standard)
0 comments:
Post a Comment