Taison-Wellington
Kane:Diego Maradona ameishauri klabu yake ya zamani ya Napoli kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane,22 ikiwa itaamua kumuuza mshambuliaji wake wa sasa Muargentina Gonzalo Higuain,30.(Piuenne)
Depay:West Ham imeungana na vilabu vya Paris Saint-Germain, Monaco na Liverpool katika mbio za kuisaka saini ya winga wa Manchester United Mdachi Memphis Depay22.(transfermarketweb).com
Falcao:Roma imefungua mazungumzo na Monaco kwa ajili ya kutaka kumsajili mshambuliaji Mcolombia Radamel Falcao,31.Ripoti toka Italia zinadai ili kufanikisha dili hilo Falcao atatakiwa kupunguza mshahara wake wa £100,000 kwa wiki.(Daily Mirror)
Taison:Arsenal imeripotiwa kuanza kuwatolea macho ya kutaka kuwasajili nyota wawili wa Shaktar
Donetsk Wabrazil Taison na Wellington.
Fellaini:AS Roma imeripotiwa kuandaa kitita cha £15m ili kumsajili kiungo wa Manchester United Marouane
Fellaini,28.(Gazzetta dello Sport)
Haidara:Chelsea ina matumaini makubwa ya kuipiku Bordeaux katika mbio za kuiwania saini ya kinda toka Mali Amadou Haidara.Haidara,17 ana milikiwa na shule ya kukuza vipaji ya JMG Academy.(L’Equipe)
Rodgers: Swansea imeripotiwa kuwa tayari kumpa kocha wake wa zamani Brendan
Rodgers ofa ya £4m kwa mwaka ili arejee kuifundisha.(The Sun)
Chamberlain:Kaka mdogo wa winga wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain aitwaye Christian Oxlade-Chamberlain amepewa mkataba wa kwanza wa kulipwa na klabu yake ya Portsmouth.(Daily Star)
Boyko:Everton imeripotiwa kuandaa £4m kwa ajili ya kumsajili mlinda mlango asiye na nafasi katika klabu ya Besiktas Mukraine Denys Boyko ili kuchukua nafasi ya Tim
Howard anayetarajiwa kuondoka mwishoni mwa msimu huu.
Martinez: Mlinzi wa kati wa Real Sociedad Inigo Martinez,24 ameachana na mpango wa kutaka kuhamia Liverpool na badala yake amesaini mkataba mpya wa kuendelea kubakia Anoeta.(AS)
Mahrez:Mshindi wa tuzo ya PFA Mualgeria Riyad,25 Mahrez ameripotiwa kukataa ofa ya kutua Paris Saint-Germain kwa madai kuwa ana mapenzi makubwa na ligi kuu ya England.
Vermaelen:Barcelona imeripotiwa kujiandaa kuwatupia virago walinzi wake watano hapo mwishoni mwa msimu huu.Walinzi hao ni Douglas, Adriano,Dani Alves na Thomas Vermaelen pamoja na Marc Bartra.
0 comments:
Post a Comment