Turin,Italia.
Juventus imeendelea kuukaribia ubingwa wake wa tano mfululizo wa Ligi ya Italia maarufu kama Seria A baada ya jumapili usiku kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya timu iliyoko mkiani ya Palermo.
Mabao ya Juventus yamefungwa na Sami Khedira (10'), Paul Pogba (70),Juan Cuadrado (73 ) na Simone Padoin (89 )
Kufuatia matokeo hayo Juventus iko kileleni na pointi zake 79,Napoli imashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 70,Roma ni ya tatu ikiwa na pointi 65.
Matokeo mengine ya Seria A,Fiorentina imeichapa Sassuolo 3-1 kwa mabao ya Gonzalo Rodriguez,Josip Ilicic na bao la kujifunga la mlinda mlango Andrea Consigli.Lazio ikiwa nyumbani Stadio Olimpico imeifunga Empoli 2-0 kwa mabao ya Antonio
Candreva kwa mkwaju wa penati na Ogenyi Onazi.
0 comments:
Post a Comment