728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, April 30, 2016

    HIZI HAPA HABARI KUBWA 10 ZA USAJILI TOKA BARANI ULAYA JUMAMOSI YA LEO APRILI 30

    Victor Valdes 

    Valdes:Mlinda mlango Muhispania Victor Valdes amerejea katika klabu yake ya Manchester United baada ya mkataba wake wa mkopo katika klabu ya Standard Liege ya Ubelgiji kuvunjwa.Liege imesema imeamua kuvunja mkataba wa Valdes,34 ili kutoa nafasi kwa wachezaji vijana.(Manchester Evening News)

    Mascherano:Kiungo wa Barcelona Muargentina Javier Mascherano,31 amekataa ofa ya €50m toka klabu moja ya China kwa madai kuwa bado ana nguvu za kuendelea kucheza Ulaya.(Mundo Deportivo)

    Courtois:Mlinda mlango wa Chelsea Thibaut Courtois huenda akatimka msimu ujao baada ya kocha mpya wa klabu hiyo Muitaliano Antonio Conte kusema iwapo ofa nzuri itakuja basi mlinda mlango huyo wa zamani wa Genk auzwe. (Daily Mirror)

    Martinez:Kocha wa Everton Roberto Martinez amesema timu hiyo haiwezi kuteteleka hata kama nyota wake wawili Romelu Lukaku na John Stones wataamua kuondoka mwishoni mwa msimu huu. (Daily Mirror)

    Ruiz:Manchester United imeripotiwa kuwa katika uongozi wa mbio za kumuwania kinda mwenye kipaji wa Real Madrid Pedro Ruiz.(Daily Star)

    Gradel:Vilabu vya Inter na  West Ham vimeingia katika vita kali ya kumuwania winga wa Bournemouth Max Gradel mwenye thamani ya £10 million.( Daily Mail)

    Gabriel:Manchester United imeripotiwa kutaka kumsajili kinda mwenye kipaji wa Parmeiras ya Brazil Gabriel Jesus,19 mwenye thamani ya £18.8m.Mbali ya Manchester United vilabu vingine vinavyomtaka Gabriel ni Real Madrid,Bayern Munich,Barcelona na Paris Saint Germain.(O'jogo)

    Mourinho:Mtandao wa Sky Sport umeripoti kuwa hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa kati ya Manchester United na Jose Mourinho juu ya kocha huyo Mreno kuchukua kibarua cha Louis Van Gaal.

    Pato:Klabu ya Corinthians inamatumaini kuwa mshambuliaji wake Alexandre Pato atabaki klabu ya Chelsea msimu ujao hii ni kutokana na kuwa nyota huyo wa zamani wa AC Milan ni kipenzi cha kocha mpya ajaye klabuni hapo Muitaliano Antonio Conte.(The Mirror)

    Walcott:Kocha mpya wa Manchester City Muhispania Pep Guardiola amemuweka katika orodha ya wachezaji atakaowasajili winga wa Arsenal Muingereza Theo Walcott,27.(Telegraph )




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI KUBWA 10 ZA USAJILI TOKA BARANI ULAYA JUMAMOSI YA LEO APRILI 30 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top