Tunis,Tunisia.
Sakata la maamuzi mabovu katika mchezo wa soka limeendelea kuchukua sura mpya karibu kila pande za dunia hasa katika bara la Afrika ambalo linapambana usiku na mchana kuhakikisha linafanikiwa kama mabara mengine.
Katika kuonyesha kuwa jambo hilo linaumiza,baadhi ya vilabu vimedirika hata kuwapinga waziwazi baadhi ya waamuzi wanaopangwa kuchezesha michezo yao na vingine hata kufikia hatua ya kususia michezo mbalimbali
SIKIA HII!!Klabu ya El Gawafel Sportives de Gafsa imetangaza kujitoa katika ligi daraja la kwanza nchini Tunisia maarufu kama Ligue 1 baada ya kuchoshwa na uonevu toka kwa waamuzi
Akitangaza uamuzi huo makamu wa Rais wa El Gawafel Sportives de Gafsa bwana Rabii Belkhodja amesema wameamua kujitoa kutokana na uonevu waliofanyiwa na mwamuzi Yassin Harush katika mchezo wao wa Jumapili dhidi ya Club Africain ulioisha kwa Gafsa kuchapwa mabao 2-1 ugenini.
Belkhodja amesema " Yassin Harush ametuonea vya kutosha.Kabla ya mchezo dhidi ya Club Africain tulipinga mapema kuteuliwa kwake kwa kuwa tulijua haya yangetokea.Ameinyima timu yetu ushindi pamoja na pointi tatu muhimu ambazo zingetusaidia katika vita ya kukwepa kushuka daraja.
Tukiwa tunaongoza kwa bao 1, Harush aliizawadia penati ya ajabu Club Africain.Penati hiyo iliwarudisha mchezoni wapinzani wetu na hatimaye wakapata bao la ushindi dakika ya 83.Hatuwezi kuendelea na ligi yenye waamuzi wa ajabu kiasi hiki.Alimaliza Belkhodja.
Gafsa iko nafasi ya15 na pointi zake 19 huku Club African iko nafasi ya 6 baada ya kufikisha pointi
26 katika michezo 23.
0 comments:
Post a Comment