London,England.
Wakati timu za wanaume za Chelsea na Arsenal zikishindwa kupata ushindi katika michezo yao ya ligi kuu iliyopigwa wikendi iliyoisha jana jumapili timu zao wa wanawake zimetinga hatua ya fainali ya michuano ya kombe la FA baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya Manchester City na Sunderland.
Chelsea ilihitaji dakika 120 ili iweze kutinga hatua ya finali baada ya kuichapa Manchester City 2-1 shukrani kwa mabao ya Fran Kirby na So-
yun,Manchester City wakijifariji kwa bao la Jane Ross.
Katika mchezo mwingine wa nusu fainali Arsenal ikiwa pungufu imefanikiwa kutinga fainali kwa mara ya 13 baada ya kuichapa Sunderland kwa jumla ya mabao 7-0.
Danielle van de Donk alifunga mabao matatu (hat-trick),Dan Carter mabao mawili,mengine yakifungwa na Fara Williams na Jordan Nobbs.
Mchezo wa fainali utapigwa jumamosi Mei 14 katika dimba la Wembley.
0 comments:
Post a Comment