728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, April 17, 2016

    HIZI HAPA HABARI 9 KUBWA ZA USAJILI BARANI ULAYA JUMAPILI YA LEO

    Jay Z

    Na Paul Manjale

    Rashford:Rapa Jay Z kupitia kampuni yake ya uwakala ya Roc Nation Sports ameripotiwa kuisaka saini ya kuwa mwakilishi wa mshambuliaji kinda wa Manchester United Marcus Rashford,18.Roc Nation Sports tayari imeshaanza kazi na bondia Andre
    Ward na mlinzi wa Bayern Munich Jerome Boateng.(Daily Mail)

    Wenger:Kocha wa Arsenal Arsene Wenger ameripotiwa kutaka kuibomoa Getafe kwa kuwasajili kwa mpigo nyota wake wawili Pablo Sarabia na Alvaro Vazquez.Sarabia, 23, na Vazquez, 24, wanaweza kupatikana kwa dau la £14m.Sarabia ni kiungo mshambuliaji,Vazquez ni mshambuliaji. (Don Balon)

    Morata:Inasemekana Manchester City itaachana na mpango wa kumsajili kiungo wa Juventus Paul Pogba na badala yake itaelekeza nguvu zake kwa kwa nyota mwingine wa Juventus Alvaro Morat mwenye mabao 10 msimu huu.(The Mirror)

    Mourinho:Gazeti la The Mirror rimeripoti kuwa Jose Mourinho amewaambia watu wake wa karibu kuwa tayari ameshakinasa kibarua cha kuwa Kocha mpya wa Manchester
    United na jukumu lake la kwanza litakuwa ni kumsajili mshambuliaji wa Napoli Gonzalo Higuain,28 mwenye thamani ya £70
    million.

    Cannavaro:Mmiliki wa Leeds United Muitaliano Massimo Cellino anamuwinda Fabio
    Cannavaro ili awe kocha mkuu mpya wa klabu hiyo inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini England.Mpaka sasa Cannavaro ameshafundisha vilabu vya Al-Ahli (Dubai), Guangzhou Evergrande (China) na Al-Nassr. (Daily Mail)

    Karius:Everton imeanza kumfukuzia mlinda mlango wa Mainz ya Ujerumani Loris Karius,21 ili kuchukus nafasi ya Tim Howard anayejiandaa kutimkia Colorado Rapids ya Marekani.Karius ana thamani ya 10m.(Sunday
    People)

    Braithwaite: Kocha wa Crystal Palace Alan Pardew ameanza kumfukuzia mshambuliaji wa Toulouse Mdenmark Martin Braithwaite,24 mwenye magoli 11 msimu huu baada ya kuchoshwa na ubutu wa washambuliaji wake Emmanuel Adebayor, Dwight Gayle na Connor Wickham.(The Mirror)

    Tete:Manchestet Utd na Juventus zimeripotiwa kuingia katika vita ya kuisaka saini ya mlinzi wa Ajax Kenny Tete mwenye thamani ya £5m.(Daily Mirror)

    Allardyce:Sam Allardyce amesema ataacha kuinoa Sunderland kama itashuka daraja na wakati huohuo atafikiria kustaafu ukocha baada ya kuhudumu kwa miaka 25 katika kazi hiyo.(Daily Mirror)


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI 9 KUBWA ZA USAJILI BARANI ULAYA JUMAPILI YA LEO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top