Barcelona,Hispania.
Barcelona imeanza kutengeneza jezi za msimu mpya wa 2016/17 bila ya kuwa na nembo ya mdhamini kifuani.
Hatua hii imekuja baada ya uongozi mpya wa miamba hiyo ya Catalunya kushindwa kufikia makubaliano ya kusaini mkataba mpya na mdhamini wake wa sasa, shirika la ndege la Qatar,Qatar Airways.
Mapema mwezi Machi Makamu wa Rais wa Barcelona anayeshughulika na masuala ya masoko Manel Arroyo alitangaza kuwa tayari wameshafanya mazungumzo na kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Nike na kuiagiza kuwa isiweke nembo yoyote katika jezi zitakazotumika mwanzoni wa msimu mpya mpaka hapo jambo hilo litakapokuwa limepatiwa ufumbuzi.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Barcelona katika kipindi cha miaka kumi kuvaa jezi zisizo na nembo ya mdhamini.Mara ya kwanza kwa Barcelona kuvaana jezi zenye nembo ya mdhamini ilikuwa ni msimu wa 2005-06.
Kabla ya kuingia mkataba na Qatar Airways,Barcelona iliwahi kudhaminiwa na Unicef pamoja na Qatar Foundation.
0 comments:
Post a Comment