Nairobi, Kenya.
Shirikisho la soka nchini Kenya FKF,limetangaza kanuni mpya za kukabiliana na vurugu za mara kwa mara wakati wa michuano ya ligi kuu ya soka nchini humo.
Hatua hii inakuja baada ya mashabiki wa Gor Mahia na AFC Leopards hivi karibuni
kuwavamia waamuzi na kuwapiga wakati wa michuano ya ligi kuu.
Mashabiki wa vlabu hivyo viwili mara kwa mara wamekuwa wakitumia nguvu, dhidi ya waamuzi kwa madai kuwa hawakubaliana na maamuzi yanayochukuliwa dhidi ya timu zao.
Suala hili la vurugu kwa vilabu hivi viwili,limesababisha wafadhili wakuu wa vlabu hivi vikongwe nchini Kenya Sportspesa.Rais wa FKF Nick Mwendwa amesema anaamini kanuni hizi zitasaidia pakubwa kupambana na hali hii ambayo wachambuzi wa soka wanaona inatia doa soka la Kenya.
Kanuni hizo zinazoanza kutekelezwa mara moja ni pamoja na:-
* Kutakuwa na Kamati maalum itakayokuwa huru kusimamia michuano ya AFC Leopards na Gor Mahia. Vlabu hivi havitaruhusiwa tena kuteua mawakala wa kusimamia usalama wa mashabiki.
* Mchezaji ambaye atachochea mashabiki kumvamia mwamuzi na kuvuruga mechi atafungiwa mechi nne na kutozwa faini ya Shilingi za Kenya 20,000 na akirudia tena kosa hilo, atafungiwa kwa mwaka mmoja kutocheza soka.
* Mchezaji au afisa wowote wa klabu akimvamia mwamuzi au akijaribu kufanya hivyo, atafungiwa kwa kipindi cha mwaka mmoja na atalazimika kugharamia matibabu ya mwamuzi aliyeshambuliwa.
* Klabu ambayo mchezaji husika atakuwa ametenda kosa hilo, itapoteza mchuano huo kwa mabao 2 kwa 0, watapokonywa alama sita na kucheza mchuano ujao wa nyumbani bila mashabiki.
* Ikiwa klabu hiyo itajikuta
katika kosa hilo ikiwa na adhabu hii, itacheza michuano mitatau ijayo bila ya mashabiki na ikirudia tena kwa mara ya tatu, itashushwa daraja na kutozwa faini Shilingi za Kenya 500,000.
* Shabiki atakayebainika amehusika na vurugu uwanjani atafungiwa kabisa kufika uwanjani kote nchini.
0 comments:
Post a Comment