728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, April 27, 2016

    MAN CITY,REAL MADRID ZATOKA SARE TASA ETIHAD

    Manchester, England.

    Manchester City imeshindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani wa Etihad baada ya Jumanne usiku kulazimishwa sare ya bila kufungana na Real Madrid katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

    Manchester City iliyokuwa bila ya kiungo wake Muivorycoast Yaya Toure ilishindwa kutumia pengo la Real Madrid kumkosa Cristiano Ronaldo kwa kupata ushindi ambao ungeipa matumaini ya kucheza fainali kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.

    Shujaa katika mchezo wa jana alikuwa ni mlinda mlango Manchester City Muingereza Joe Hart ambaye aliinyia Real Madrid bao la ugenini baada ya kuokoa michomo ya hatari hasa toka kwa Pepe.

    Timu hizo zitarudiana tena wiki ijayo huko Santiago Bernabeu na mshindi atakata tiketi ya kucheza fainali mwezi Mei huko San Siro,Italia.

    Vikosi.
     
    Man City:
    Hart, Sagna , Kompany, Otamendi ,Clichy,Fernandinho , Fernando, Jesus Navas (Sterling 75), De Bruyne, Silva,(Iheanacho 40), Aguero. 

    Real Madrid:
    Navas, Carvajal, Sergio Ramos, Pepe,Marcelo, Modric, Casemiro 6, Kroos 7,(Isco 90), Lucas, Benzema,(Jesse 46)

    Nusu fainali ya pili itapigwa leo Jumatano ambapo Atletico Madrid watakuwa nyumani Vicente Carderon kuialika Bayern Munich.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAN CITY,REAL MADRID ZATOKA SARE TASA ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top